
Serikali yake tayari inaendelea na utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.6
Kupitia miradi hiyo tayari Tanroads imekamilisha kwa asilimia 100 miradi 25 ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1,198 iliyogharimu Sh. trilioni 1.68 katika kipindi cha utawala wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pekee.
Pia hadi sasa tsh. bilioni 101.1 zimelipwa kwa wakandarasi katika miradi 24 ya ujenzi wa barabara inayoendelea kutekelezwa pamoja na miradi minne ya ujenzi wa viwanja vya ndege nchini.
Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja inaendelea kwa kasi maeneo mbalimbali nchini na hakuna mradi uliokwama kwa sababu Serikali imekuwa ikilipa wakandarasi kulingana na mikataba.
0 Comments