LICHA YA KUWEPO KWA CHANGAMOTO YA UHAMIAJI HARAM BADO USALAMA MKOA WA KIGOMA WAIMARIKA

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amesema hali ya usalama mkoani hapa imeendelea kuimarika pamoja na uwepo  wa changamoto ya idadi kubwa ya wahamiaji haramu kutoka nchi zinazopakana na mkoa, wanaolenga kuingia nchini kujitafutia kipato sambamba na ukosefu wa hali ya amani na utulivu maeneo wanayotoka.

Sirro ametoa kauli hiyo alipokutana  Kamishna  wa Polisi Jamii CP.  Faustine Shilogile  akiwa mkoani hapa kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa wa Polisi Jamii Kanda Namba tano inayohusisha mikoa ya Kigoma, Kagera na Tabora.

Balozi Sirro ameuomba  uongozi wa Serikali kupitia jeshi hilo kuendelea kuongeza watendaji katika mkoa,  kutokana na  uhitaji mkubwa uliopo.

Upande wake Kamishna Shilogile amesema serikali inaendelea kuchukua hatua  katika kuboresha utendaji kazi wa Jeshi hilo ikiwemo kuongeza kwa kiasi kikubwa nyenzo sa usafiri ili kurahisisha ufikiwaji wananchi na kutatua changamoto zao za kiusalama.




Post a Comment

0 Comments