KATAMBI AFANYA MKUBWA MKUBWA WA KUSHUKURU WANANCHI SHINYANGA MJINI

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM. - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, amefanya mkutano mkubwa wa hadhara kuwashukuru wananchi kwa imani waliyoionesha katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa kumchagua tena kuwa mbunge, kumpigia kura nyingi za ushindi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwachagua madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mkutano huo wa kihistoria umefanyika Februari 22, 2026 katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga, ukihudhuriwa na maelfu ya wananchi, wanachama wa CCM na viongozi wa serikali na chama, hali iliyoakisi mshikamano mkubwa wa kisiasa katika Mkoa wa Shinyanga.

Akihutubia umati huo, Katambi alitoa shukrani zake za dhati kwa wananchi kwa kuendelea kumuamini na kuipa ushindi CCM, akisisitiza kuwa ushindi huo ni wa wananchi wote wanaotamani maendeleo na ustawi wa taifa.
“Nawashukuru sana wananchi wa Shinyanga kwa kuniamini na kunichagua tena niwe mbunge wenu, pamoja na kumpigia kura nyingi za ushindi Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025. Nawahakikishia kasi ya maendeleo inaendelea,” amesema Katambi.

Amesema ataendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo kwa kusimamia miradi ya maendeleo katika sekta za miundombinu, maji, afya, elimu na ajira kwa vijana, akieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia imeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi.

Kwa mujibu wa Katambi, ndani ya miaka minne ya uongozi wa Awamu ya Sita, miradi mikubwa ya kimkakati imetekelezwa ikiwemo ujenzi wa madaraja, reli ya kisasa (SGR), barabara, shule na hospitali, sambamba na program za kuinua uchumi wa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Katika kuonesha msimamo wa serikali katika usimamizi wa miradi, Katambi alimuonya mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa pamoja na barabara ya lami kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kuongeza kasi ya ujenzi huo.
“Ukicheka na nyani, utavuna mabua, haiwezekani Rais anatoa pesa za miradi ya maendeleo, lakini wakandarasi wachache wanataka kuzichezea. Kwa cheo changu nilichonacho cha Waziri wa Mambo ya Ndani, mtaipata fresh,” ameonya Katambi.

Aidha, amewataka wakandarasi wote jimboni humo kuheshimu mikataba yao na kukamilisha miradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, huku akiwaonya watumishi wazembe na wanaojihusisha na rushwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi.

Katika kusisitiza suala la amani, Katambi amewahimiza wananchi kuendelea kulinda na kudumisha umoja na utulivu wa nchi.

“Bila amani hakuna maendeleo,” amesisitiza, akiongeza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao ili kuweka mazingira bora ya uwekezaji na kukuza uchumi wa Taifa.
Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Shinyanga Mwanahamisi Munkunda na Mjumbe wa SADC akizungumza.

Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mwanahamis Munkunda, amesema Serikali ya CCM chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari imeanza kutekeleza ahadi zake, akitaja utoaji wa ajira katika sekta za elimu na afya ndani ya siku mia za mwanzo, kuanza kwa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote pamoja na kuendelea kwa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, amempongeza Katambi kwa kuendelea kuaminiwa na Rais na kumtaka kushughulikia changamoto ya upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kusogeza huduma karibu na wananchi katika ngazi ya kata.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wameipongeza Serikali kwa juhudi za maendeleo na kuomba kuimarishwa kwa miundombinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa hadhara Mjini Shinyanga, akitoa shukrani kwa imani waliyoionesha katika Uchaguzi Mkuu kwa kumchagua kuwa Mbunge, kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kuwachagua madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).  
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Patrobas Katambi, akihutubia wananchi wa Shinyanga katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kwa imani yao ya kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM.

Post a Comment

0 Comments