Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) CDE. Sikunjema Shabani amewataka wananchi wa Kata hiyo kumpigia kura za kishindo kumchagua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani ameleta maendeleo mengi katika nchi yetu.
Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa mwanamke wa kwanza kuidhihirishia Tanzania kwamba wanawake wanaweza na wanatakiwa wajivunie kuwa wanawake.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni amesema kwamba ameleta maendeleo mengi hasa mradi wa Dp World ambao umetufikia kata yetu ya Somangira lakini pia ukitaka kuvuka kivuko cha feri unachagua wewe mwenyewe mwananchi utumie usafiri upi na kwa gharama unazozichagua wewe mwananchi.
Kwa upande wake mgombea Udiwani Kata ya Somangira Luja Juma Ally amesema kwamba Rais wetu katika Kata ya Somangira kuna miradi mingi kwa kipindi alichoongoza.
Amesema kwamba endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo ataendeleza pale viongozi wenzake waliotangulia na walipobakisha kwani wamefanya kazi kubwa za maendeleo katika Kata yao na atasimamia maendeleo kwa umakini mkubwa kwa sababu uwezo anao kwa kuwa ameshakua kiongozi kwa muda mrefu hivyo atahakikisha analeta maendeleo katika kata hiyo.
Anaomba kukipa ridhaa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa ndio kinacholeta maendeleo kwa ujumla kwenye nchi yetu lakini hata katika Kata hiyo.
Aidha amesema kwamba Kata ya Somangira imekuwa na changamoto nyingi zinazowakabili hasa baadhi ya maeneo hayana shule, zahanati lakini pia barabara zake ni korofi hivyo atahakikisha kutatua changamoto za miundombinu kwa kujenga hoja kwa kushirikiana na madiwani wenzake kwenye mapato ya ndani kugawana kile kinachopatikana kitekeleze matakwa yanayotakiwa.
Ameahidi kwamba miradi yote itakayopelekwa Somangira atasimamia kwa uaminifu mkubwa kwa sababu Mama yetu anapambana usiku na mchana kusaka pesa kwa ajili ya sisi watanzania.
Pia amesema kwamba anatambua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo kuna fursa mbalimbali zinazoelekezwa katika kata hiyo hasa miradi mbalimbali ya ujenzi wa madaraja hivyo atawapambania vijana wenzake kwenda kufanya kazi hizo.
Atashuka kwenye mikutano ili kutatua kero za wakazi na atapokea kero kupitia mikutano ya hadhara na yeye atazifanyia kazi kwa kushirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa.
Alisema kwamba atalia nalo usiku na mchana na upotevu wa maeneo ya kijamii kwani ni maeneo muhimu kwani popote lilipo eneo la jamii kama hayajaendelezwa ataenda kuyafanyia mkakati wa aina yake ili kuyapa kipaumbele ili wananchi waweze kutambua haki zao.
Pia kuna changomoto ya mikopo kwani kuna baadhi ya makundi yanapata mikopo huku wengine kukosa, yeye atasimamia vilivyo makundi hayo ili wote wapate mikopo hiyo lakini pia atasisimamia mikataba wanayopatiwa bodaboda ili waweze kupata haki zao kutokana na mikataba yao.



0 Comments