Ni zamu ya Sanga, Mungu akisema ndio, hakuna wakusema hapana

Mgombe wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Haran Nyakisa Sanga amesema Serikali ya awamu ya sita imetoa jumla ya shilingi bilioni 325, kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.

Pia amesema yeye ni Mbunge wa Wananchi ambaye anasikiliza matatizo ya Wananchi, anajadiliana nao na anatafuta suluhisho la changamoto hizo.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Somangira Sanga amesema leo amekuja kuwauliza wenyewe, kwa kuwa kigamboni inamatatizo mengi sana ya miundombinu hususani barabara kati cha ya changamoto zilizopo ni ipi iwe kipaumbele cha kwanza baada ya oktoba 29.

Anasema kuwa wakimpa kura za kutosha atakwenda Bungeni akiwa na ajenda kubwa moja ambayo ni barabara ili kumaliza changamoto ya miundombinu ya barabara.

“Lakini ndugu zangu ninaelewa nimejaribu kupita kidogo katika mitaa yetu watu wa mtaa wa Sala wanamatatizo na uhitaji wa soko, nikapita nikaambiwa watu wa mkwajuni wanashida ya umeme toka nguzo zimewekwa nyaya hazisogei, nichagueni  nikaharakishe uwekaji wa nyaya kule mkwajuni” alisema Sanga.

Ameongeza kwa kusema kuwa Kata ya Somangira inachangamoto ya upungufu wa vituo vya afya, pomoja na shule, ili kumaliza changamoto hizo oktoba 29, kura zote ni kwa CCM, sababu ndio chama kinachoweza kumaliza changamoto hizo.

Haran amesema kwamba pia anaelewa kuwa Somangira kunachangamoto kubwa sana ya miundombinu ya maji, kuna sehemu zina maji na kuna sehemu hazina maji.

“Mwaka 2022 mwezi wa 11, Dkt. Samia alikuja Kigamboni na kuzindua tanki la maji la liata milioni 15, katika Kata ya Kidarawe II na uzinduzi ule alisema “ nawahakikishia wanakigamboni mtapata maji kwa asilimia 100” naombeni mnichague nikasimamie hiyo asilimia 100, ya maji safi na salama.

Aidha amesema kuwa wamchague Luja kuwa Diwani wa Kata ya Somangira pamoja na yeye ili wakashughulikie changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Amesema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Samia ni mwanamke shujaa, hodari na anaweza kusimamia na kuleta maendeleo makubwa Tanzania.

“Ni waambieni hakuna zawadi kubwa tutakayo weza kumpa huyu mama kama kumpa kura za kishindo, tarehe 29, wewe dada, wewe kaka twendeni tukampe kura za kishindo ninawaambieni kama mtaenda kutoa kura za kishindo mtakuwa mmenisaidie mimi Mbunge kumkumbusha wakati nadai fedha za maendeleo katika jimbo la Kigamboni” alisema Haran.

Mkimpigia kura za kutosha nitakuwa na nguvu za kumkumbusha Dkt. Samia kuwa wale Wanasomangira walikupa kura elfu 30, wanaomba barabara, wanaomba maji na mengine mengi.

“Chondechonde tumpe kura za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassani, ukimpa kura za kishindo ndio namna pekee unayoweza kusema mimi huyu mama nilimchagua” alisema Nyakisa.

Amesema ukipiga kura utakuwa umetimiza jambo la msingi la kumchagua kiongozi, lakini unapata haki ya kudai maendeleo.

“Ndugu zangu naombeni sana tusifanye majaribio,  hata tukichukua tochi ukaweka betri tatu umeme unawaka, ukichukua betri mbili ukaongeza na kibunzi umeme hauta waka kwaiyo tujitahidi sana oktoba 29, tukapige kura” alisema Sanga.

Hata hivyo amemaliza kwa kusema kuwa akichaguliwa atafanya mikutano ya adhara , lakini lazima tufanye kazi na dawa, tule, tunywe tufanye bata ili kuhakikisha akili zetu zinakaa sawa.

Post a Comment

0 Comments